Karibuni sana Rose Education Centre

Rose English Medium school ni mojawapo ya shule bora zilizoko katika mkoa wa Kilimanjaro. Shule ni ya Bweni na kutwa kwa wanafunzi wa darasa la chekechea hadi darasa la saba.

Tuna eneo zuri la shule lenye muonekano wa kuvutia, na lenye majengo mazuri na waalimu wenye sifa kubwa ya ualimu na wanaotoa elimu bora kwa watoto kuanzia chekechea mpaka darasa la saba.
Tunazidi kuangalia hatua za mbele na mipango bora kwa maendeleo ya shule yetu. Tuna uhakika kuwa Rose Education Centre ni shule bora kwa maendeleo ya mtoto wako.

rose-education-centre-shule

Shule inatoa huduma za ziada kwa wanafunzi wake kama ifuatavyo:

  • Huduma za michezo, mpira wa miguu pamoja na wamikono, riadha na michezo ya ndani [indoor games]
  • Tunatoa vikundi vyamijadala katika masuala mbalimbali ili kuwapa wanafunzi uwezo wa kuchambua na kujenga hoja katika masomo

Karibuni wote tujenge maisha bora ya watoto wetu.

 

Mimi mtiifu

Rose_sahihi
Roselyne Swai

Mwanzilishi na Mkurugenzi