Ushirikisho wa Anam Cara Network pamoja na shule ya sekondari iitwayo Franz-Ludwig huko Bamberg, Ujeremani


 

 

 

Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwangu, nilipokutana na marafiki wapya wawili kutokea Ujerumani. Ilikuwa ni mwezi wa tatu mwaka 2009. Tuliweza kujuana kwa undani na waliweza kujua mipango yangu ya mbele katika kituo hiki kwani walipenda na walitaka kunisaidia ili ndoto zangu ziweze kutimia. Marafiki hawa ni Friederike Klein na Thomas Kovacic. Hawa marafiki wanaendesha Shirika lisilo la kiserikali liitwalo Anam Cara Network. Hivyo tulianza ushirikiano mkubwa.

rose-education-centre-barikiwe

rose-education-centre-vifaa

Anam Cara Network

 

 

Kila mwaka walinitembelea mimi na watoto wa Rose Education Centre na tulizungumza mengi kwa kirefu kujua mahitaji ya shule na maendeleo ya shule kwa ujumla.

Mwaka 2011, mwezi wa kumi na moja, Shirika la Anam Cara Network lilianza kusaidia kuingiza umeme shuleni na kuingiza maji masafi yenye kina kirefu kwa kwenda chini kwa mita 60. Na pia waliendelea kusaidia shule kwa kununua vifaa na vitabu vya walimu vya kufundishia na vitabu vya wanafunzi vya kujifunzia. Pia waliendelea kusaidia ujenzi uliokuwa haujakamilika na kufanya ukamilike kwa kiwango kikubwa.

Mwezi wa tatu, mwaka 2015, Shirika la Anam Cara Network lilisaidia shule kuweza kununua basi kubwa la shule ili kuweza kubeba wanafunzi wa kutwa.


Mabadilishano

 

 

Mwaka huo huo wa 2011, walinialika nchini Ujerumani ambapo nilikwenda na mwalimu mmoja wa chekechea. Nilitembelea taasisi mbalimbali za kielimu kama chekechea mbalimbali na hata shule za juu. Tukio moja kubwa kwangu ni pale nilipotembelea shule ya juu huko Bamberg. Shule hii ni kubwa sana nchini Ujerumani inayofundisha watoto zaidi ya 1000. Susanne Heim, mmoja wa walimu katika shule hiyo, ni mwanachama pia wa Anam Cara Network alianzisha na kuendeleza mahusiano kati ya shule ya Rose Education Centre na Shule kubwa ya Franz-Ludwig Gymnasium huko Bamberg nchini Ujerumani.

ushirikiano-na-shule


rose-education-centre-mkutano-na-walimu

Shule ya sekondari Franz-Ludwig, Ujeremani

 

 

 
Mwezi wa tisa, mwaka 2015, walimu wawili na wanafunzi 17 walitembelea shuleni Rose Education Centre kama matokeo mazuri ya mahusiano mazuri ya shule kwa shule. Mahusiano haya ya Anam Cara Network na shule ya Franz-Ludwig Gymnasium yalileta mafanikio makubwa kwa shule ya Rose Education Centre na kuifanya shule kupata maendeleo ya haraka na kuonekana shule ya kisasa.


Mkutano wa wazazi na walimu

 

 

Kwa sasa wazazi wa watoto wanakutana katika vikao vya wazazi na kujadili mambo mbali mbali ya kimaendeleo yahusuyo shule. Walimu pia wanapata mafunzo ya ufundishaji kutoka kwa Susanne Heim na timu yake yote ili ujuzi wa ufundishaji uzidi kuongezeka na kupata maendeleo ya kasi kubwa na kuzidi kuongeza ujuzi kwa walimu na wanafunzi wao.

Tuna tumaini kuwa kwa kipindi kijacho kutakuwa na nafasi nzuri kwa wanafunzi wetu na walimu kutembelea marafiki nchini Ujerumani.

rose-education-kongamano-la-walimu