Maelekezo ya kujiunga na shule ya awali


 

 

 

 

Nachukua fursa hii kukupongeza kwa kuchagua kujiunga na shule hii ya Rose Education Centre. Shule hii ni ya kutwa na bweni, mchanganyiko.

Nakukaribisha sana Rose Education Centre nikiwa na matumaini kwamba utajifunza na kusoma kwa bidii ili Taifa lifaidike kupata kiongozi hodari hapo baadaye.

Pamoja na pongezi hizo napenda kukufahamisha kwamba kazi ya kusoma ni ngumu na siyo lelemama. Kwa kipindi chako chote cha uanafunzi katika shule hii itabidi ujinyime mambo mengi ya anasa, na kutumia muda wako mwingi kwa kusoma na kujitoa kwa nguvu zako zote na kwa kutumia kwani “Elimu ni ufunguo wa maisha na vile vile Elimu ni Mkombozi.” Baada ya kugundua siri hii kubwa ya masomo Uongozi wa shule Walimu na Wafanyakazi wako tayari kukusaidia katika kufanikisha hilo.

rose-education-centre-bwalo-la-chakula

rose-education-centre-bweni

Maelezo kuhusu shule

 

 

 

Masomo yanayofundishwa ni:- Kiswahili, Kiingereza, Hisabati, Sayansi, Jiografia, Historia, Uraia, Haiba na michezo na Stadi za Kazi, na masomo yote ya chekechea. Vile vile nimeambatanisha sheria za shule (baadhi tu) heshima, na nidhamu ya shule, makosa ya kufukuzwa shule, sare ya shule (muhimu) kuripoti shuleni, lugha ya mawasiliano shuleni kama kiwanda angalizo na ahadi ya mzazi na mwanafunzi. Ahadi ya utii na fomu ya vipimo ili uyapitie kwa maana ya kuyasoma na kuyaelewa.


Mahitaji ya jumla kwa kila mwanafunzi

 

 

Ada kwa wanafunzi wa kutwa ni kama ifuatavyo:

  • Kwa mwaka ni TSH 600,000
  • Kwa muhula ni TSH 200,000

Ada kwa wanafunzi wa Bweni ni kama ifuatavyo:

  • Kwa mwaka ni TSH 900,000 na kwa muhula ni TSH 300,000
  • Ada inaweza kulipwa kwa namna tatu yaani ada ya mwaka mzima, ada ya nusu mwaka au ada ya robo mwaka.
rose-education-centre-basi-la-shule

rose-education-centre-mstarini

Sare ya shule

 

  • Kwa wanafunzi wa kutwa Sare zinapatikana shuleni kwa gharama ya TSH. 65,000
  • Kwa wanafunzi wa Bweni ni TSH 100,000

 

Wavulana:

  • Suruali mbili nyeusi
  • Shati mbili nyeupe za mikono mifupi pamoja na tai
  • Sweta moja nyeusi
  • Sare mbili za kushindia shuleni

Wasichana:

  • Sketi mbili nyeusi
  • Shati mbili nyeupe mikono mifupi na skafu ya shingoni
  • Sare mbili za kushindia shuleni
  • Sweta moja nyeusi

Muhimu

 

 

 

 

Hatutapokea fedha yoyote hapa shuleni. Fedha ipelekwe Benki ya BARCLAYS katika akaunti Namba 0176001798 – ROSE EDUCATION CENTRE iliyoko Mjini Moshi usisahau kuandika jina la mwanafunzi na darasa.

rose-education-centre-nyumba-ya-walimu

rose-education-centre-jengo-la-shule

(1) Ndoo 2 za lita 10
(2) Mkebe wa vifaa vya hisabati (Mathematical set)
(3) Madaftari ya kutosha kwa muhula mzima yasiyopungua 12 kwa madara ya juu aina ya Counter books quire 3, na 20 kwa madarasa ya chini

Mahitaji mengine

(4) Godoro la futi 3 x 6 – nchi 4
(5) Mashuka mawili ya bluu
(6) Kandambili za kuogea
(7) Chandarua ya futi 4 x 6 ya square kwa madarasa ya chini na round kwa madarasa ya juu (Darasa la 3 mpaka la 7)
(8) Sabuni ya kuogea za medicated soap kama dettol, Protex, n.k.
(9) Sabuni ya unga kilo nne (sadolini 1) na miche 5 aina ya Jamaa tu siyo nyingine pamoja na soap dish.
(10) Dara ya meno paketi kubwa 1 aina ya white dent na siyo nyingine
(11) Miswaki 3 ya size ya kati
(12) Mafuta ya kujipaka aina ya Vaseline kopo kubwa 3
(13) Chana ya nywele
(14) Malapa pea mbili
(15) Begi la shule la kuhifadhi madaftari
(16) Taulo kwa kuogea
(17) Chupi zisizopungua nne kwa wavulana
na wasichana
(18) Kalamu za wino za kutosha zisizopungua 15 kwa muhula mzima
(19) Kiwi nyeusi kopo kubwa 2
(20) Mwavuli wa saizi ya kati kwa ajili ya mvua
(21) Sahani ya bati kijiko na kikombe cha plastic


Mipaka ya shule

 

 

 

Mwanafunzi haruhusiwi kutembea sehemu zifuatazo isipokuwa kwa ruhusa
maalumu:

 

a) Chumba cha walimu (Staff Room)
b) Ofisi za shule
c) Maabara

rose-education-centre-ofisi-ya-walimu

rose-education-centre-darasani

Kuripoti shuleni

 

 

 

Mara tu ufikapo shuleni nenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Makamu Mkuu wa shule ambaye atakupokea na kukagua vifaa vyako.

Mawasiliano yote ndani ya shule kati ya mwalimu na mwanafunzi na kati ya mwanafunzi na mwanafunzi yatakuwa kwa lugha ya kiingereza kama ilivyo lugha ya kufundishia.